Quantcast
Channel: Swahili Time
Viewing all articles
Browse latest Browse all 571

Historia Fupi ya Marehemu Captain Komba!

$
0
0
 Mbunge wa Mbinga na Msanii maarufu, Captain John Komba, alifariki dunia leo katika hospitali ya TMJ mjini Dar es Salaam, kutokana na athari za ugonjwa wa kisukari. Mwenyezi mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.
The late Captain John Komba


Historia Fupi ya Marehemu John Komba
Marehemu Kaptain Komba alizaliwa Marchi 18 mwaka 1945 alipata elimu ya msingi huko nchini Tanzania katika shule ya Lituhi baadae elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya Songea iliyopo kusini mwa Tanzania kuanzia 1971 hadi mwaka 1974.

Mwaka 1975 hadi mwaka 1976 Marehemu John Komba alijiunga na chuo cha ualimu kilichopo Kleruu Iringa, Kusini Magharibi mwa Tanzania ambapo alihitimu cheti cha ualimu.

Marehemu John Komba ni mwanajeshi ambaye alipata mafunzo ya uafisa wa Jeshi katika chuo cha Maafisa wa Jeshi kilichopo Monduli kaskazini mwa Tanzania mwaka 1977 hadi mwaka 1978.

Keptain John Komba pia alipata mafunzo mengine ya siasa kutoka chuo Kikuu cha Washngton International ambapo alitunukiwa shahada ya siasa mwaka 2006 hadi mwaka 2008.


**********************************************************************

Waziri wa Ardhi,William Lukuvi (wa kwanza kushoto) akimfariji mke wa marehemu, Salome Komba

Khadija Kopa akilia kwa Uchungu nyumbani kwa Komba.
 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 571

Trending Articles